Mlinda mlango kutoka nchini Hispania, David De Gea huenda akawa
amebakisha saa 48 za kurejea kwenye lango la Man Utd, baada ya kuonekana
yupo tayari kwa kazi hiyo.
De Gea anapewa nafasi kubwa ya kurejea langoni mwake baada ya
kushikiwa nafasi hiyo na mlinda mlango kutoka nchini Argentina Sergio
Romero, kutokana na utimamu wa kimwili na kiakili alionao kwa sasa.
Mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 29, amekua akifuatiliwa na
meneja wa Man Utd akiwa kwenye kambi ya timu ya taifa ya Hispania, na
alionekana mwenye furaha wakati wote licha ya janga la kushindwa
kujiunga na Real Madrid mwishoni mwa mwezi uliopita kuonekana kumsumbua.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti la Daily Star la nchini England
umebaini kwamba pamekua na mazungumzo kati ya meneja huyo na De Gea na
hali inaonekana kuwa shwari kwa hivi sasa.
Louis Van Gaal, alionyesha kuhofia kumpa nafasi De Gea ya kukaa
langoni mwanzoni mwa msimu huu, kutokana na fikra za uhamisho wake wa
kurejea nyumbani na kujiunga na Real Madrid kuonekana kumsumbua kwa
kiasi kikubwa tangu walipokua kwenye michezo ya kujiandaa mwezi July.
Endapo De Gea atapewa nafasi ya kurejea langoni mwishoni mwa juma
hili, itakua ni kipimo kizuri kwake kuonyesha amejitengeneza kiakili na
kimwili, kutokana na uzito wa mchezo ambao unawakabili Man Utd nyumbani
ambapo watapambana na Liverpool.
Sergio Romelo ambaye alisajili kama mchezaji huru amesema na mwenendo
mzuri katika lango la Man Utd tangu katika mchezo wa mwanzoni mwa msimu
huu dhidi ya Spurs ambao walikubali kufungwa bao moja kwa sifuri, kisha
mchezo dhidi Aston Villa waliokubali kufungwa bao moja kwa sifuri na
baada ya hapo mashetani wekundu wakatoka sare ya bila kufungana dhidi ya
Newcastle Utd, kabla ya kufungwa mabao mawili kwa moja.
Post a Comment