Takribani siku 10 tangu uhamisho wake wa kwenda kujiunga na klabu ya Real Madrid kukwama, golikipa wa timu ya taifa ya Spain na klabu ya Manchester United, David De Gea amefanya maamuzi kuhusu hatma yake ndani ya klabu hiyo ya Uingereza.


 
David de Gea amesaini mkataba mpya wa kuendelea kubaki Manchester kwa miaka mengine minne baada ya mkataba wake wa sasa kuisha mwakani.
Golikipa huyo mwenye miaka 24 alianza mazungumzo ya mkataba mpya baada ya uhamisho wake ambao ungegharimu kiasi cha  £29million kushindikana siku ya mwisho ya dirisha la usajili.
 
Muda mfupi uliopita kupitia mtandao wa Twitter, De Gea alitumia akaunti yake kutangaza mkataba wake mpya na Manchester United.
Mkataba mpya wa De Gea utamfanya kuwa golikipa anayelipwa zaidi kwa kulipwa mshahara usiopungua kiasi cha £200,000 kwa wiki.

Post a Comment