Ni wiki moja imepita toka Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu duniani (FIFA) Sepp Blatter hatuhumiwe kwa makosa kadhaa na ofisi ya mwanasheria mkuu Uswiss. Blatter ametuhumiwa kwa makosa ya kuingia mikataba mibovu ya matangazo ya haki za TV akiwa pamoja na Rais wa zamani wa CONCACAF  Jack Warner mwaka 2005.

Blatter anatuhumiwa kwa kosa la kumlipa Rais wa Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA Michel Platini pound milioni 1.3 mwaka 2011 ikiaminika fedha hizo zilitumika kufanyia kampeni za Sepp Blatter ili aendelee kuwa madarakani na kosa jingine ni utawala mbovu. Wengi walitamani kufahamu baada ya tuhuma hizo atajiuzulu mara moja au atafanya nini?.
Sepp-Blatter-007
September 28 Blatter ameingia kwenye headlines baada ya kujibu tuhuma juu yake kwa kueleza mambo kadhaa ikiwemo suala la yeye kumlipa pound milioni 1.3 Michel PlatiniBlatter >>> “Sikufanya chochote kinyume cha sheria au isivyo kawaida kiasi cha pound milioni 1.3 zililipwa kama fidia na sio vinginevyo”
Sepp Blatter ambaye ana umri wa miaka 79 bado ataendelea kuwa Rais wa Shirikisho hilo licha ya tuhuma hizo zinazomkabili kwa sasa. Blatter amekuwa Rais wa FIFA tokea mwaka 1998 ndio aliingia madarakani kwa mara ya kwanza.

Post a Comment