Mtoto wa Diamond Platinumz, Tiffah ameundiwa kamati maalum kwa
ajili ya kuratibu shughuli ya sherehe yake ya kufikisha siku arobaini
tangu azaliwe, inayotarajiwa kufanyika Jumapili, Septemba 20.
Kwa mujibu wa gazeti la Nipashe, mama mzazi wa Diamond ndiye
anayeongoza kamati hiyo yenye wajumbe kadhaa ambao ni ndugu wa karibu wa
familia ya mwimbaji huyo.
“Tiffah anatutoa jasho shangazi zake, mimi na wanakamati wenzangu
tunaendelea kujumuika pamoja, kwa ajili ya Tiffah inabidi na sisi
tufutwe jasho Jumapoli kwa kweli,” Esma ambaye ni mdogo wake Diamond
ananukuliwa.
Pamoja na Esma na Mama Diamond, wengine wanaouna kamati hiyo ni mama mzaa chema, Zarina ‘The Bosslady’ Hassan.
Sura ya Tiffah inatarajiwa kuoneshwa kwa mara ya kwanza hadharani siku hiyo ya Jumapili, Septemba 20.
Dimond aliandika ujumbe wa kuwafahamisha mashabiki wake kuhusu siku hiyo.
Post a Comment