Vyama vya upinzani vinavyounda Ukawa vimemshukia mgombea urais wa
CCM, Dk John Magufuli kwa madai ya kutumia kauli mbiu ya vyama hivyo
katika kampeni zake.
Akiongea katika mkutano wa kampeni za za kumnadi mgombea urais
anaungwa mkono na Ukawa, Edward Lowassa, waziri mkuu mstaafu, Frederick
Sumaye alisema kuwa kitendo cha Dk Magufuli kuanza kutumia kauli mbiu za
umoja huo kinaonesha jinsi alivyoshindwa kupambana na upinzani dhidi
yake.
“Magufuli anasema hakuna mtu anayeweza kuwatisha, lakini atambue CCM
yake maji yameanza kuingilia kwenye pua sasa wanashika popote na
kutapatapa,” alisema. “Ndio maana unasikia anasema Movement For Change
yaani M4C ni Magufuli For Change, hawana haya kweli wameishiwa hoja,
hivi M4C NA Magufuli ilianza ipi?” aliwahoji wananchi walioitikia kwa
sauti ya juu ‘M4C’.
Sumaye aliongeza kuwa hali hiyo ni dalili tosha kuwa baada ya CCM
kuiongoza nchi kwa zaidi ya miaka 50, hivi sasa fikra na mawazo ya chama
hicho imefikia kikomo na kinapaswa kupumzishwa.
Hayo yanafuatia kauli ya Dk Magufuli alipokuwa mkoani Kigoma hivi
karibuni ambao aloiwaambia wananchi kuwa maana ya ‘M4C’ inayotumiwa na
Chadema ni ‘Magufuli For Change.
Kumbukumbu zinaonesha kuwa ‘M4C’ ilianza kutumiwa na Chadema mwaka
2006 kama kampeni maalum ya kuongeza hamasa ya kufanya mabadiliko katika
uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.
Post a Comment