Diamond: Alichovaa Tiffah mkononi si ‘’Hirizi’’


11820739_419258674934747_1464202425_n[1]


Diamond amezungumza na Clouds E ya Clouds TV alipoulizwa kwanini amemvalisha mtoto wake hirizi wakati kipindi hiki ni cha ‘kidigitali’.

‘’Naomba mjue alichovishwa mtoto wangu si hirizi,hiki kitu kinaitwa ‘mvuje’ aliyoivaa mkononi hata mimi unaniona leo Diamond nilivalishwa na karibu watoto wengi Tanzania na nchi za Kiafrika wakizaliwa lazima wafungwe ile kwahiyo ulimwengu huu wa kidigitali usitufanye tukasahau au kudharau kabisa mila zetu ambazo ndio zimetukuza’’alisema Diamond

‘’Na simaanishi hii ni ya kishirikina iko hivyo ndiyo ishakuzwa kwenye desturi hizo na sidhani kama ina dhambi yoyote kwa mtazamo wangu, mimi kwa sababu mimi niliwekwa mama yangu aliwekwa na kizazi changu mimi kiliwekwa kwahiyo hawa wakina Chriss Brown ninaowaangalia hawawezi kunipumbaza nikafanya nisahau nilipotoka,’’aliongeza Diamond.

Post a Comment