Aliyekuwa Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania Jaji Joseph Sinde Warioba amesema kwamba Mgombea Urais wa CCM Dr. John Pombe Magufuli ni mtu muadilifu, Mchapakazi na Asiyekuwa na tamaa hivyo anazikaribia sifa za Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Akizungumza
na wananchi kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika juzi mjini Bunda,
Warioba alisema Dr. Magufuli ndiye anayestahili kuwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kati ya wagombea nane kutoka vyama mbalimbali
vilivosimamisha wagombea kwani mpaka kufika kwake hapo hakujatokana na
fedha wala harufu ya fedha yeyote.
Alidai
kuwa Vyama vya upinzani vilitakiwa kusimamisha wagombea wao wenyewe
bila kuazima kutoka Chama cha Mapinduzi CCM jambo ambalo linawaondolea
sifa za siasa zao za upinzani wa kweli nchini.
Post a Comment