.
.
Ni stori ya kisiasa ambayo ilianza kuchukua headlines kwenye mitandao mbalimbali kuhusu wasanii wawili wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel na Vicent Kigosi aka Ray kuondoka UKAWA na kuhamia chama cha Mapinduzi.


Baada ya taarifa hizo kuchukua nafasi kubwa kwenye mitandao sasa ripota wa millardayo.com amezungumza na  Steve Nyerere ambaye ni mwenyekiti wa kampeni ya Mama ongea na Mwanao…’Ndugu zetu wakina Vicent Kigosi na Aunt Ezekiel walitoroka wamerudi CCM  kabla hawajatangaza lakini watatangaza wamerudi kwa kishindo kikubwa wanaamini bila hapo walipofika bila nguvu ya Mh Jakaya Mrisho Kikwete wasingiweza kufika‘ – Steve Nyerere
.
.
‘Kwa hiyo nataka kuwaambia watanzania kuwa hao watu wamerudi katika chama cha mapinduzi na wala msidanganywe pilika pilika za huku na kule hawa watu ni wanachama wa CCM hai walitoroka na sifa ya kutoroka ni kukosa nidhani kwa sisi wazazi ambao tuna watoto , mtoto akitoroka unatakiwa umpe adhabu ili siku nyingi afahamu njia ya sahihi na njia sahihi ni chama cha Mapinduzi ambacho kina Dkt John Pombe Magufuli na Mama Samia Suluhu’ – Steve Nyerere

Post a Comment