Mgombea urais wa UKAWA Mh Edward Lowassa amesema akichaguliwa kuwa rais ataanzisha benk maalumu kwa ajili ya kusadia makundi maalumu yaliyosahaulika likiwemo la wachimbaji wadogo wa madini, mama lishe, na bodaboda na wamachinga.

 

Kabla ya kufika Shinyanga mjini Mh Lowasa alifanya mikutano katika jimbo la Kishapu, Asolwa, na Kahama, ambapo baada ya kupata mapokezi ya kishindo anaanza kumwaga sera na kufafanua jinsi atakavyo zitekeleza.
 
Kilio cha wananchi kupewa ahadi zisizotekelezwa kikaendela kuwa ajenda 22kuu ambayo Mh Lowassa na wagombea wa nafasi zingine wanaelezea watakavyozikabili kama wananchi wakichagua viongozi wa UKAWA

Post a Comment