Wakati
baadhi ya vyama vya siasa vikionyesha kuwa na wasiwasi kufuatia
kuondolewa ama kubadilishwa kazi kwa baadhi ya watendaji wa tume ya
taifa ya uchaguzi mwenyekiti wa tume hiyo jaji mstaafu Damiani Lubuva
amevitaka kuacha kuingia utendaji wa tume hiyo kwani tume haiongozwi kwa
maagizo ya wanasiasa.
Mwenyekiti huyo ameyasema hayo alipokutana na watu wanaoishi na
ulemavu na kusema kuwa mabadiliko yanayofanyika ni ya kiutendaji tuu na
wala hayana uhusiano wowote na jinsi ambavyo wanasiasa hao wanavyosema
kuwa ni mbinu za kutaka kuiba kura.
Naye katibu mkuu wa shirikisho la watu wenye ulemavu kutoka
Kilimanjaro Bw Kawawa Salim amesema watu wenye ulemavu wa kusikia
wanashindwa kufuatilia mikutano ya kampeni kutokana na kukosekana
wakarimali na hivyo kushindwa kujua ahadi zinazotolewa na wagombea.
Awali akitoa mada katika mkutano huo kaimu mkurugenzi wa tume Bw
Emanueli Kavishe amesema kwa sasa tume imejipanga vyema na hasa katika
vitambulishio vya kupigia kura ambavyo ni vya kisasa na mtu hawezi
kuvihujumu kiurahisi.
Post a Comment