Jeshi
la Polisi mkoani Singida lina mshikilia mkazi moja wa mkoa wa Tabora
wilaya ya Igunga wa kijiji cha Itumba kwa tuhuma za kukutwa na viungo
vya binadamu na nyara za serekali.
Akiongea na wandishi wa habari kamanda wa jeshi la Polisi mkoani
Singida ACP Thobias Sedoyeka amemtaja mtuhumiwa kuwa ni Bwana Magida
Bundala aliyekuwa akitokea mkoani Tabora kuja mkoani Singida kuwa
salimia ndugu zake ambayo walikuwa wamewekwa maabusu katika kituo cha
polisi cha wilaya ya Ikungi.
Kamanda Sedoyeka amesema mbinu waliyo tumia kumkamata mtuhumiwa
huyo ni baada ya askari kumtilia mashaka na kuamua kumkagua wakati
akisubiri kuwasalimia ndugu zake ambao ni maabusu na kukuta vipande
viwili vya fuvu la binadamu, ngozi ya chatu, vipande vya ngozi ya simba,
pembe ambayo haija julikana na chupa tatu za mafuta ya simba.
Kwa upande wao baadhi ya wakazi wa manispaa ya Singida wameliomba
jeshi la Polisi kuhakikisha, linamfuatilia mtuhumiwa huyo ili kuweza
kubaini mtandao mzima kwa sababu za imani potofu ikiwemo kupata madaraka
wana sababisha vifoo vya binadamu ikiwemo wenye ulemavu wa ngonzi
Albino.
Katika hatua nyingine kamanda Sedoyeka amesema jeshi la Polisi
mkoani Singida lina washikilia watu wanne wakiwemo mwalimu moja wa shule
ya sekondari msungua, mwalimu wa shule ya msingi Italala na wakazi
wawili wa kijiji cha msimihi kwa tuhuma za kujiandikisha mara mbili
katika daftari la kudu la wapiga kura.
Post a Comment