Mtu moja amefariki na wengine watano kujeruhiwa baada ya kuzuka vurugu za kisiasa katika jimbo la Tarime mkoani Mara na gari la mgombea wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema Ester Matiku kuharibiwa vibaya.


Katibu wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema Chacha Heche amesema aliye uwawa ni mfuasi wa Chadema ambapo chanzo cha kuuwa ni vurugu zilizo anzishwa na vijana wa CCM wakati wa kizuia mapokezi halali ya mkutano wa wagombea wa Chadema kata na jimbo ambapo vijana hao waliwavamia kwa mapanga na ndipo wakamchoma kada wa Chadema kwa kitu chenye ncha kali na kufariki dunia muda mfupi. 
 
Kufuatia tukio hilo jeshi la polisi limetoa taarifa ya maandishi iliyo sainiwa na kamanda wa polisi Lazaro Mambosasa ambapo amekiri kutokea kwa tukio la mauaji hata hivyo katika hali isiyo ya kawaida jeshhi hilo limezuia waandishi kupiga picha gari la mgombea wa jimbo la Tarime Ester Matiko lililo haribiwa vibaya kwa mapanga ambapo waganga wa hospitali ya rufaa Tarime wamethibitisha kupokea majeruhi na maiti.
 

Post a Comment