Muimbaji kiongozi wa kundi la Yamoto Band, Asley Isihaka amefiwa na mama yake mzazi ambaye alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari.


Taarifa za msiba huo zimethibitishwa na meneja wa Yamoto Band, Said Fella. Kwa mujibu wa Fella, mama Asley alikuwa anasumbuliwa na Presha na Kisukari na jana usiku alizidiwa na kukimbizwa hospitali ambapo alifariki majira ya alfajiri.

Mjuaji tz inatoa pole kwa Asley, ndugu jamaa na wote walioguswa na msiba. Mungu awape faraja katika kipindi hiki kigumu.

   Source  Dar24

Post a Comment