Kampeni za uchaguzi mkuu zimezaa mbwembwe kadhaa zinazokoleza mchakamchaka huo. Mbwembwe hizo zimepelekea kuzaliwa kwa jina jipya la mgombea ubunge wa Muleba Kusini kupitia CCM, Profesa Anna Tibaijuka.


Jina hilo jipya limekuwa kivutio cha wafuasi wa CCM ambapo huzua shangwe pale anapotambulishwa mgombea huyo na viongozi wakuu wa chama chake.

“Tumemleta kwenu mgombea supa wa ngazi ya ubunge, huyu diye ‘karandalugo’ anayetibu magonjwa yote, huyu ni mama wa mfano na anajua matatizo yote, ni mpambanaji siu zote , sio mwingine bali ni profesa Anna Tibaijuka,” alisikika mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kagera, Costancia Buhiye.

‘Karandalugo’, ni jina la dawa ya kienyeji ambayo inasadikika kutibu magonjwa mengi ya binadamu na hutumiwa sana na wakazi wa mkoa wa Kagera. Hivyo, Tibaijuka anatajwa kama ‘Karandalugo’ wa matatizo ya wakazi wa jimbo hilo.

Post a Comment