Aliyekua mlinda mlango wa klabu za Tanzania Prisons, Moro United, Yanga SC, St.George ya Ethiopia, African Lyon, Bandari FC na Gor Mahia FC za Kenya, Simba SC na timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Ivo Mapunda amelaani vikali tabia ya Juma Nyosso ya kuwadhalilisha wachezaji wenzake kwa kuwashika sehemu za makalio.
“Binafsi nachukua nafasi hii kuwaomba wachezaji wenzangu, wanaocheza na waliowahi kucheza soka, wadau wote pamoja na mashabiki wa ndani na nje ya nchi KULAANI kwa nguvu zote tabia na vitendo vya aibu na udhalilishaji anavyofanya mchezaji mwenzetu Nyosso” ameandika Ivo katika ukurasa wake wa facebook.
“Hii ni aibu, siyo yake pekee bali ni yetu sote wachezaji hasa wa medani ya kimataifa.
Tunaonekana ‘hopeless’ pia na hata kukosa nafasi ya kwenda nje ya kucheza soka kutokana na tabia dhalimu. Tunaomba adhabu yake itakayotolewa iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hii. Wanajifunza nini watoto au vijana wanaochipukia katika soka kwa huu udhalilishaji ukizingatia Nyosso ni mchezaji mkubwa?”
Post a Comment