Chama cha NCCR mageuzi jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro kimelaani vikali kitendo cha madiwani wa chama cha Demokrasia na maendeleo chadema kukata kumuunga mkono mgombea ubunge jimbo la Vunjo ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa vyama vinavyounda katiba ya wananchi UKAWA Bw.James Mbatia kwa tuhuma za kusimamisha wagombea madiwani kila kata.

Akitoa taarifa kwa waandishin wa habari katibu mwenezi wa chama cha NCCR Mageuzi jimbo la Vunjo Bw.Stanley Temba amesema kitendo kinachofanywa na madiwani wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) ni kinyume na makubaliano kwa kuwa lengo la muungano wa vyama hivyo ni kupata ushindi kuanzian ngazi za chini hadi urais.
 
Amesema mgawanyiko huo utaasababisha wananchi kukosa imani na viongozi wa vyama vinavyounda ukawa na kwamba ni vema madiwani hao wakaacha hasira badala yake kukaa  pamoja na kujadiliana ili kuondoa kasoro zilizojitokeza badala ya kumsusia mgombea ubunge jimbo la Vunjo kwa tiketi ya NCCR Bw.James Mbatia.
 
Naye mjumbe wa halimashauri kuu wa chama cha NCCR Mageuzi taifa Bw.Hemed Msabaha amekiri kuwa chama hicho kimesimmisha wagombea udiwani katika kata zote kwa madai kuwa viongozi wa chama hicho ndiyo wanakubalika zaidi katika jamii ikilinganishwa na chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema.
 
Hata hivyo juhudu za kuwapata viongozi wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema mkoa wa kilimanjaro kuzungumzia sakata hilo zinaendelea.
 

Post a Comment