Siku zote nitahakikisha nakusogezea kila stori inayonifikia na hapa stori ninayotaka kukupatia ni hii kutoka kwa mtayarishaji Sheddy Clever ambaye alizichukua headline hivi karibuni baada ya kutayarisha single mpya ya Diamond na staa kutoka Marekani Neyo.
Mtayarishaji huyo alipokutana na ripota
wa millardayo.com leo Sept 10 aliweza kuzungumzia collabo hiyo na jinsi
Diamond alivyomfundisha Neyo maneno ya kiswahili katika single hiyo
mpya.
‘Kwanza kabisa nimefurahi baada ya
Diamond Platnumz kuniambia kuwa nahitaji kwenda Nairobi kwenda
kutayarishaji single yake mpya aliyomshirikisha Neyo kwa kweli nashukuru
sana uongozi mzima wa WCB wakina Babu Tale na Diamond kwani sikuwahi
kuwaza kuja kufanya kazi na Neyo, miongoni mwa single zake
ninazozikubali ni ule wa So Sick’ – Sheddy Clever
‘Siwezi
kuzungumzia ni maadhi gani ya wimbo walioufanya ila watu wakae tu mkao
wa kuupokea single hiyo mpya, kama vile watu mnavyojua Diamond amekuwa
akijituma kwa hali na mali kuinua soko letu la Tanzania hasa kwenye
upande wetu wa muziki neyo kaimba Kishwahili katika single hiyo Diamond
alimuimbisha Kiswahili siwezi kusema ni maneno gani ya kiswahili bali
watu wakae mkao wa kula’ – Sheddy Clever
Post a Comment