Kocha wa Arsenal Arsene Wenger, ametoa utetezi wake juu ya
kushindwa kununua mchezaji wa ndani katika dirisha la usajili
lililofungwa hivi karibuni, akisema kuwa hakukuwa na mchezaji ambaye
klabu ilikuwa na uhitaji naye.
Vijana hao wenye maskani yao kwenye jiji la London, walimsajili
kipa Petr Cech tu kutoka Chelsea mapema kabisa wakati dirisha la usajili
limefunguliwa, hali iliyojenga imani kubwa kwa mashabiki juu ya ubingwa
wa EPL msimu huu, lakini hata hivyo hakuna usajili mwingine
uliofanyika.
Wenger alihusishwa na tetesi za kumsajili mshambulaiji wa Real
Madrid Karim Benzema lakini hata hivyo mpaka dirisha linafungwa hakuna
kilichotokea.
Wenger aliwaambia waandishi: “Mwishoni, suluhisho lilikuwa si kama
tulivyaka. Tuliangalia kwa makini lakini hakukuwa na suluhisho sahihi.
“Hebu angalia katika soko la wachezaji kwa sasa, utaona kwamba kuna
upungufu mkubwa sana wa wachezaji. Suluhisho tulilokuwa nalo halikuwa
na ushawishi kabisa.
“Habari njema kuhusu dirisha ka usajili, sasa limefungwa rasmi na tunachokiangalia kwa sasa ni kucheza mpira tu”.
Post a Comment