Saratani si tu  kwamba ni ugonjwa  hatari lakini pia ni ugonjwa unaompa mwanadamu mateso makali. Haijalishi ni saratani ya ngozi, ya tumbo au ya kizazi.

 Vilevile ni ugonjwa ambao matibabu yake yanahitaji gharama kubwa mno. Inasemekana kuwa mgonjwa mmoja wa saratani ambaye saratani yake imechelewa kugundulika, huhitaji kiasi cha Sh 300,000 kwa ajili ya matibabu.

 Tatizo jingine ni kuwa kutokana na elimu duni, Watanzania wengi hushindwa kupima saratani na kuigundua mapema hivyo hugundulika katika hatua za mwisho.

Leo tutachambua kwa undani ukubwa wa tatizo hili kwa kuangalia ni ugonjwa wa hatari kiasi gani.

Melanoma ni saratani ya hatari sana kwa maisha ya mwanadamu. Ni mara chache sana saratani hii hushambulia watu lakini inapotokea mtu akapata saratani hii basi maisha yake yanakuwa hatarini sana.

Saratani hii si rahisi kuigundua ukilinganisha na saratani nyingine za ngozi nilizokwisha taja hapo juu.

Siyo tu kwamba saratani hii ni ngumu kidogo kuitambua lakini pia husambaa haraka zaidi kuliko saratani nyingine za ngozi.

Melanoma huweza kusambaa na kushambulia viungo vingine zaidi ya ngozi kama mifupa na ubongo. Inapofikia hatua hii saratani hii inakuwa ngumu sana kutibika.

Dalili za Melanoma

Dalili ya kwanza kabisa ambayo inabidi kila mtu afahamu ni kubadilika kwa ukubwa, rangi au ule muundo wa alama ya ngozi ambayo umekuwa nayo kwa muda mrefu au umezaliwa nayo. Alama hii ni ile ambayo ina rangi nyeusi zaidi ukilinganisha na maeneo mengine ya ngozi.

Mabadiliko haya si lazima yawe yanatokea haraka haraka yanaweza kuwa yanatokea taratibu katika kipindi cha miezi lakini cha muhimu ni kuwa unaona kabisa mabadiliko kwenye alama hiyo ya ngozi.

Post a Comment

  1. Habar mimi ngozi yangu imeanza kutokwa na vitone vidogo vyeupe na mimi ni mweusi na huwa naona kama inaongezeka naomba kujua nini hasa kinacho nisumbua

    ReplyDelete