MICHEZO BLATTER AGOMA KUJIUZULU FIFA A+ A- Print Email Rais wa shrikisho la soka duniani Sepp Blatter amesema kuwa hatojiuzulu wadhfa wake licha ya mashtaka ya uhalifu yanayofungiliwa dhidi yake na wachunguzi wa Uswizi. Blatter ambaye ni raia huyo wa Usiwizi aliye na umri wa miaka 79, anatuhumiwa kutia saini kwenye mikataba ambayo haikuifaa FIFA mbali na kufanya malipo yasiokubalika kwa rais wa shirikisho la UEFA Michel Platini Blatter ambaye atajiuzulu kama rais wa FIFA mwezi Februari anasema kuwa hajafanya kosa lolote kinyume na sheria.Katika taarifa iliotolewa na mawakili wake,Blatter amesema kuwa pauni milioni 1.5 zilizotolewa kama malipo kwa Platini ,ambaye ndio kiongozi wa shrikisho la soka barani Ulaya UEFA mwaka 2011 ni halali na hakuna zaidi. Wakati huo huo Platini mwenye umri wa miaka 60,amendika barua kwa wanachama wa UEFA akikana kufanya kosa lolote.Wawili hao pia wanakabiliwa na uchunguzi na kamati ya maadili ya FIFA kuhusu malipo hayo ambayo Platini anasema yalikuwa ya kazi wakati alipokuwa mshauri wa kiufundi wa Blatter kati ya mwaka 1999 na 2002.
Post a Comment