Kampeni za Uchaguzi Mkuu zinaendelea ambapo jana mgombea urais
kupitia Chadema anayeungwa mkono na vyama vya upinzani vinavyounda
Ukawa, Edward Lowassa alikuwa Muleba ambapo alifanya mkutano mkubwa wa
kampeni uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi wa eneo hilo.
Lowassa alionesha kushangazwa na umati mkubwa uliojitokeza kwenye
mkutano huo na kuonesha jinsi alivyofurahishwa na kuridhishwa na
mahudhurio hayo aliyoyaita ‘maajabu’.
Akiwashukuru wananchi hao, Lowassa alieleza kuwa hakutegemea kama
angepata mapokezi makubwa kama hayo mjini Muleba, “Sikujua kama mna
mahaba makubwa kiasi hiki.”
“Tumepita maeneo mbalimbali nchini hali niliyoikuta ni kama hii hapa
ya Muleba, Mungu anipe nini mie, asanteni sana,” alisikika Lowassa.
Aidha, aliwaomba kura wananchi hao akiahidi kuwaletea maendeleo kwa kasi na kupambana na umasikini uliokithiri.
Aliwasihi wananchi hao kuhakikisha wanafanya maamuzi sahihi kwa
kumchagua ili wapate mabadiliko ya kweli kwenye maisha yao. Alisisitiza
kuwa endapo atapewa ridhaa ya watanzania atahakikisha elimu bure kuanzia
darasa la kwanza hadi chuo kikuu inaanza kutekelezwa kuanzia January
mwaka huu.
Post a Comment