Msafara
wa mgombea wa nafasi ya urais wa Chadema anayeungwa mkono na vyama
vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA, Mh.Edwrad Lowassa
umejikuta ukizuiwa mara kwa mara na mamia ya wakazi wa wilaya za Korogwe
na Handeni wakati alipokuwa akitoka Tanga kuelekea jijini Dar es
Salaam.
Msafara huo wa mgombea wa nafasi ya urais Mh.Edwrad Lowassa haikuwa
rahisi hata kidogo kufika mapema jijini Dar es Salaam akitoa jiji Tanga
baada ya mamia ya wananchi kuvamia mara kwa mara msafara huo katika
barabara kuu.
Lakini tukataka kujua dhamila kuu ya wananchi hawa kuvamia msafara wa mgombea huyo wa nafasi ya urais.
Akiwa mjini Korogwe akalazimika kusitisha msafara wake na kuamua kuwaleza nini atalifanyia jiji la Tanga punde atakapochaguliwa.
Msafara huo uliokuwa ukiongozwa na jeshi la polisi kutoka Tanga
hadi Dar es Salaam ulisimamishwa mara kwa mara na wakazi wa maeneo ya
Muheza, Korogwe, Michungwani, Kabuku, na Mkata ambapo walitumia fursa
hiyo kumueleza changamoto zinazowakabili.
Hatimaye Mh.Edward Lowassa na msafara wake wakalazimika kuzungumza
na maelfu ya wakazi hao Muheza, Korogwe Michungwani, Kabuku, Mkata.
Post a Comment