Mgombea
wa nafasi ya urais kupitia Chadema anayeungwa mkono na vyama vinne
vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA, Mh.Edwrad Lowassa
amelazimika kuahirisha mkutano mjini Tanga baada ya maelfu ya wakazi
waliojitokeza kushindwa kuenea ndani ya uwanja wa Tangamano jijini
Tanga.
Kwa mara ya kwanza ndani ya jiji la Tanga shughuli zote
zinazofanyika katika mitaa ya barabara ya 4, 5,6,7, 8 zililazimika
kusimama kwa muda baada ya maelfu ya wakazi wa jiji hilo waliojitokeza
katika uwanja wa Tanagmano, hali iliyopelekea kushindwa kuendelea kwa
mkutano huo.
Licha ya juhudi zilizofanywa na viongozi wa UKAWA wakiongozwa
Fredrick Sumaye za kujaribu kutuliza hali ya mambo kushindikana jambo
lililomlazimu Mh.Edward Lowassa kulazimika kusitisha mkutano huo.
Je? Nini kauli ya Chadema baada ya mkutano huu kuvunjika, John Mrema ni meneja kampeni wa Chadema.
Uamti huo wa wakazi wa jiji la Tanga ulionekana dhahili ulionekana
dhahili kuwashinda maafisa wa taasisi ya mslaba mwekundu redcros mjini
Tanga.
Akiwa jiji Tanga katika siku yake ya kwanza ya kampeni alifanya
mikutano katika maeneo ya Bumbuli Mombo kabla ya kuhitimisha katika
uwanja wa Tanagmano mjini Tanga ambapo aliahidi kuboresha sekya ya afya
ndani ya siku miamoja baada ya kuapishwa.
Post a Comment