Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema kuanzia sasa itaanza kubandika matokeo ya kura za urais kwenye vituo vya kupigia kura katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu ili kuongeza uwazi na kupunguza malalamiko ya wizi wa kura.
Mpango
huo umeelezwa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji mstaafu
Damian Lubuva alipozungumza na viongozi wa dini jijini Dar es Salaam
ambao walimueleza hoja hiyo kuwa moja ya vigezo vitakavyokamilisha
mchakato huo kwa amani na utulivu na kuwaridhisha wagombea na wafuasi wa
vyama.
Alisema
licha ya kubandikwa vituoni, utangazaji wa matokeo utafanyika kama
kawaida katika kila ngazi, udiwani kwenye kata, ubunge wilayani na urais
Tume makao makuu.
Jaji Lubuva aliwahi kunukuliwa siku za nyuma akisema kuwa “hakuna
haja ya kuwa na shaka wala kuandaa vijana wa kulinda vituo. Hakutakuwa
na nafasi hiyo kwa sababu kura zote zitahesabiwa na kubandikwa huko.
“Kila
mtu atajua diwani gani kapata kura ngapi, na mbunge na hata rais
aliyemchagua. Itakuwa tofauti na zamani ambapo zilikuwa zinasafirishwa
na kuhesabiwa wilayani ambako watu wengine walidhani yanabadilishwa,” alisema.
Post a Comment