Baada ya mapumziko ya takribani siku 14, ligi kuu ya England maarufu kama Barclays Premier League imeendelea mchana wa leo kwa mchezo mkali kati ya Chelsea dhidi ya Everton.


 
Mchezo huo uliopigwa katika jiji la Liverpool ndani ya uwanja Goodison Park umemalizika kwa Chelsea kuambulia kipigo kingine kwa kufungwa 3-1.
 
Magoli matatu ya mshambuliaji Naismith yametosha kuipa Everton ushindi mzito dhidi ya vijana wa Jose Mourinho.
 
Naismith alianza kufunga katika dakika ya 17, dakika 5 baadae akaongeza la pili kabla ya Matic hajaifungia Chelsea goli la kufutia machozi.
Dakika 8 kabla ya mchezo kumalizika Naismith akashindilia msumari wa mwisho na kuipa ushindi wa 3-1 Everton.

Post a Comment