Rais Jakaya Kikwete ameeleza nia yake ya kumtaja mmiliki wa kampuni
ya Richmond iliyohusika katika ufisadi wa tenda ya ufuaji wa umeme wa
dharura mwaka 2007/08.
Rais Kikwete aliweka wazi nia yake hiyo jana katika viwanja vya Lake
Tanganyika mkoani Kigoma alipokuwa anawaaga wananchi wa mkoa huo, ambapo
alionesha kumshangaa mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu kumtaka
amtaje mmiliki wa Richmond.
Alisema anashangaa kuona Tundu Lissu anamtaka amtaje mwenye Richmond wakati anazunguka naye mikoani.
“Endapo Tundu Lissu atashindwa kumtaja mwenye Richmond, nitatoka hadharani na kumtaja mwenyewe,” alisema Rais Kikwete.
Post a Comment