Star wa Hip Hop mwenye tungo adimu Bongo, Kala Jeremiah ametoa
mtazamo wake kufuatia hatua ya baraza la sanaa Tanzania kuifungia
‘Ngoma’ ya Roma Mkatoliki ‘Viva Roma’.
Akizungumza kupitia kipindi cha ‘The jump off’ cha Times Fm, Kala
amesema kama tatizo ni ushahidi wa kile alichokiimba Roma, basi ngoma
zote zinapaswa kufungiwa kwa kuwa hazina uhalisia.
“Ushahidi gani unautaka? tuseme basi wale wanaoimba baby nakuona
kwenye glass watoe basi ushahidi wao wanamuonaje mtu ndani ya glass, coz
uimbaji ni unakuwa na fikra kwanza.
Nafikiri basata wameingilia na wanavuruga demokrasia, kwenye mziki
wetu kuwanyima watu uhuru wa kuongea, walianza kwa vitisho zamani,
kuzifungia kimya kimya sasa hivi ndio wameleta hii ya kuzifungia
waziwazi kabisa” alisema Kala.
Post a Comment