Mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa anayekipiga katika klabu ya Manchester United ya Uingereza Anthony Martial amepigwa picha na mapaparazi akishuka katika teksi akiwa pamoja na mkewe Samantha huku amembeba mtoto wake mdogo.
Anthony Martial wa Man United huu ni kama muendelezo wa maisha yake ya furaha katika jiji la Manchester
na amekuwa akionekana kutoka na mkewe kila mahali, safari hii ameshuka
katika teksi akiwa kambeba mtoto wake mikononi huku mkewe Samantha akiwa anamlipa dereva teksi.
Staa huyo wa Man United ambaye amesajiliwa na Man United kwa ada ya uhamisho wa pound milioni 36 akitokea klabu ya Monaco ya Ufaransa, bado hajapewa nyumba ya kuishi na anaishi katika hoteli ya Lowry hivyo alipigwa picha hizo akiwa anaingia hotelini.
Licha ya kuwa Anthony Martial ni mgeni katika Ligi Kuu Uingereza, kocha wa klabu ya Manchester United Louis van Gaal
aliwahi kumtetea kwa mashabiki wasitegemee makubwa kutoka kwake, kwani
bado mapema anahitaji muda wa kuzoea Ligi, good news ni kuwa mechi yake
ya kwanza Man United alifunga goli moja dhidi ya Liverpool katika ushindi wa 3-1.
Post a Comment