Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema kuwa wananchi wa jimbo la Lushoto hawatapiga kura ya ubunge katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu kutokana na kufariki kwa mgombea kupitia Chadema, Mohamed Mtoi.


Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva alisema kuwa Tume imelazimika kuahirisha uchaguzi huo kwa kuwa sheri ya Uchaguzi inaelekeza hivyo pale inapotokea mgombea akifariki kabla ya uchaguzi.
Mgombea Ubunge, Lushoto Tanga
Marehemu Mohamed Mtoi (36) alifariki kwa ajali ya gari wiki iliyopita.  Alifariki baada  ya gari alilokuwa amepanda akitokea kwenye kampeni kuacha njia na kupinduka.

Post a Comment