Imefahamika kwamba mkali wa muziki wa hiphop kwa upande wa wanawake, Nicki Minaj ataanza kuonekana kwenye series ya vichekesho ya ABC Family.
Series hiyo inayoataandikwa na Kate Angelo inatarajiwa kuanza kuruka mwakani na dhima kuu ya comedy hiyo ni kuonyesha maisha ya Nicki Minaj tangu alipokuwa mtoto, maisha aliyopitia kabla hajakuwa staa kwenye game ya hiphop duniani.
Licha ya kuwa hii sio mara ya kwanza kwa Nicki kuonekana kwenye filamu mbalimbali, lakini ameandika kwenye ukurasa wake wa twitter na kusema kwamba hii ni nafasi nyingine kwake ya kuonyesha kwamba naye ni gwiji kwenye vitimbi.
Pia Nicki ametoa update kwamba anatafuta muigizaji atakayecheza sehemu yake pindi alipokuwa mdogo.
Hili ni shavu kwako mdada wewe ambaye unamuonekano kama wa Nicki Minaj na mwenye uwezo wa kuigiza.
Unaweza kutuma picha kwenye akaunt zake za kijamii.
Post a Comment