Mwenyekiti ya tume ya Taifa ya uchaguzi, jaji Damiani Lubuva amewaonya wanasiasa wanaotumia muda mwingi kutoa maneno mengi yenye ukakasi yaliyo kinyume na sheria ya uchaguzi mkuu.

Lubuva amevionya vyama vya siasa vinavyotumia maneno hayo badala ya kunadi sera ya vyama vyao na kueleza kuwa tume itachukua hatua kali dhidi ya vyama vinavyofanya hivyo.

Kauli hiyo ya jaji Lubuva imekuja zikibaki takribani siku 27 kabla ya watanzania hawajapiga kula kumchagua rais, wabunge na madiwani huku joto likizidi kupanda.

Wanasiasa wengi wakishuhudiwa kutoa maneno mengi makali dhidi ya wagombea wa vyama vingine hali inayotafsiriwa kinyume na utamaduni wa Tanzania pamoja na sheria za nchi

Post a Comment