Faida 5 Za Kunywa Maji Mengi
Faida 5 Za Kunywa Maji Mengi
Asilimia 60% ya mwili wa mwanadamu ni maji, lakini kiasi kikubwa cha maji hupotea mwilini kila siku kupitia mkojo, kinyesi na jasho…hivyo ni muhimu kujiwekea utaratibu mzuri wa kunya maji kwa wingi ili kuuweka mwili katika afya iliyo bora kila siku.

Katika mwili wa mwanadamu maji ni muhimu sana kwaajili ya kazi mbalimbali za kiafya na ndio sababu ya mimi kukuandikia makala hii ili uweze kuzitambua Faida 5 Za Kunywa Maji Mengi kila siku. Sasa hebu tuzame katika mada yetu kama ifuatavyo.
Usipitwe na Hii: Faida kubwa za kula kifunguakinywa cha kutosha (usizozijua)

Faida Kuu 5 Za Kunywa Maji Mengi

Faida 5 Za Kunywa Maji Mengi
Faida 5 Za Kunywa Maji Mengi

1. Maji huzipa seli za misuri afya na nguvu .

Seli za misuli yetu huhitaji kiasi cha kutosha cha maji ili kuwezesha misuli kufanya kazi katika ufanisi mkubwa. Kama mwili ukikosa maji ya kutosha seli hufanya kazi katika mazingira magumu ambayo hupelekea mtu kujisikia uchovu katika misuli. Lakini kama mwili utakuwa na maji ya kutosha mtu hatopata adha yoyote itokanayo na upungufu wa maji mwilini. Watu ambao wanafanya mazoezi mara nyingi wanaweza kushuhudia ukweli huu. Baada ya mazoezi ya muda mrefu mtu huweza kuhisi uchovu kwasababu kiasi kikubwa cha maji kimepotea kwa njia ya jasho, lakini kama mtu atapata huduma ya maji kwa haraka , kupiatia chakula ama kwa kunywa maji, ataweza tena kuurejesha mwili wake katika hali ya kawaida.

2. Maji huondoa sumu mwilini.

Figo ndio chombo kikuuu kinachohusika na kuondoa sumu mwilini, lakini figo haiwezi kufanya kazi yake vizuri bila kiasi sahihi cha maji mwilini. Sumu kuu mwilini ni Urea katika damu, Naitrojeni na taka za maji mumunyifu (water-soluble) ambazo zinaweza kuchujwa kwenye figo na kutolewa nje ya mwili kupitia mkojo na jasho. Bila maji ya kutosha mwilini mkojo hauwezi kutoka kwa urahisi pia huweza kuwa na na harufu kali, lakini kama utakunywa maji kwa wingi kila siku , utaiwezesha figo kufanya kazi yake kwa urahisi bila matatizo.
Usipitwe na Hii: Faida kubwa za kula kifunguakinywa cha kutosha (usizozijua)

3. Maji husaidia kupambana na kuvimbiwa.

Maji ni muhimu sana katika mfumo wa mmeng’enyo wa chakula (Digestion), Mtu anapokunywa maji ya kutosha husaidia chakula kupita kwa urahisi katika mirija, na hiyo inamaana kuwa unapokunywa maji ya kutosha unausaidia utumbo mpana kukipitisha kinyesi kwa urahisi baada ya mmeng’enyo. Kutokana na kukosekana kwa maji ya kutosha utumbo hulazimika kufyonza maji kutoka katika kinyesi na hatimaye hupelekea kinyesi kuwa kigumu na kuleta shida wakati wa kukitoa mwilini , jambo ambalo hupelekea kuvimbiwa.
Faida 5 Za Kunywa Maji Mengi

4. Maji hutunza afya ya ngozi na kuondoa makunyanzi.

Ngozi huhitaji kiasi kikubwa cha maji ili iweze kuwa katika afya bora bila makunyanzi. Kama hautoipa ngozi maji ya kutosha, upungufu wa maji mwilini husababisha makunyanzi na michirizi kutokea mara katika ngozi.

5. Maji husaidia mmeng’enyo wa chakula (Digestion)

Kunywa glasi ya maji dakika chache kabla ya kula kifungua kinywa au chakula cha jioni inaweza kusaidiakuharakisha mmeng’enyo wa chakula.
Usipitwe na Hii: Faida kubwa za kula kifunguakinywa cha kutosha (usizozijua)
Ninaimani umepata ujuzi wa kutosha kupitia mada yetu ya Faida 5 Za Kunywa Maji Mengi kila siku. Unashauriwa kutumia angalau glasi 8 za maji kila siku. Nawatakia kila La heri katika hilo watu wangu wa nguvu!!!

Post a Comment