Mwimbaji huyo ameeleza wazi kuwa yeye sio mfano wa kuigwa katika jamii (role model), katika mahojiano maalum aliyofanya na jarida la NME.
Kauli hiyo ya Rihanna ilifuatia maswali yaliyolenga kufahamu msimamo wake kama angefanya ziara ya muziki na mwimbaji mwenzake Taylor Swift ambapo akataa na kudai kuwa hawaendani hata kidogo. Alisema yeye na mwimbaji huyo wanatofautiana sana kwa kuwa Tailor ni mfano wa kuigwa na yeye sio.
Ni kama Rihanna amewaelekeza wanaotafuta mfano wa kuigwa katika jamii kumfuata Taylor Swift badala ya kumfuata yeye.
“’I don’t think our brands are the same: I don’t think they match, I don’t think our audiences are the same. In my mind she’s (Taylor) a role model, I’m not,” alisema Rihanna.
Post a Comment