Kampeni za uchaguzi mkuu mwaka huu zina hamasa ya aina yake huku
kila kambi ikihakikisha hailiachi jiwe lolote la upande hasimu bila
kugeuzwa.
Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema ameukejeli uamuzi wa CCM
kumchagua Wema Sepetu kuwa mwenyekiti msaidizi wa kampeni ya chama hicho
ya ‘Mama Ongea Na Mwanao’, yenye lengo la kuwashawishi akina mama
kuwaambia watoto wao waichague CCM.
“Hivi kwa nini watanzania tunadanganywa mchana kweupe na akina Wema
Sepetu na wenzake, eti wameanzisha kampeni inaitwa ‘mama ongea na
mwanao’, hivi kweli kuna mtu asiyejua tabia na mienendo ya Wema Sepetu
ilivyo!? Sasa ataongeaje na watoto wetu,” alisema Lema kwenye mkutano wa
Kampeni uliofanyika wilayani Karatu.
Wema Sepetu ni mwenyekiti msaidizi wa kampeni ya Mama Ongea na Mwanao ya CCM, iliyo chini ya uenyekiti wa Steve Nyerere.
Post a Comment