Waandishi wa habari waliohudhuria mkutano wa baada ya mchezo wa
ligi ya mabingwa barani Ulaya kwenye ukumbi wa uwanja wa Do Dragão mjini
Porto, walishangazwa na kauli ya meneja wa klabu ya Chelsea, Jose
Mourinho ambayo iliendelea kudhihirisha kikosi cha The Blues ni bora
kuliko FC Porto.
Mourinho aliutumia mkutano huo na waandishi wa habari kwa kutaka
kuujuza umma wa soka duniani kwamba kikosi chake kilikua na ubora wa
hali ya juu katika mchezo wa usiku wa kuamkia hii leo, licha ya kukubali
kisago cha mabao mawili kwa moja.
Mourinho alisema anashindwa kuamini kama kweli Chelsea wamepoteza
mchezo dhidi ya Porto na hadhani kama ilikua sahihi kwao kupoteza
mpambano huo ambao ulimrejesha nyumbani nchini Ureno tena kwenye klabu
aliyoanzia kazi ya umeneja.
Alisema anaamini hakuna kilichoharibika kwake kutokana na kuamini
kikosi chake kilicheza vyema na kudhihirisha ubora uliopo, lakini bahati
ya ushindi haikua kwao baada ya kuelekea kwa wenyeji ambao walimaliza
mchezo kwa furaha kubwa.
Post a Comment