Meneja wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger ameripotiwa kutengana na mkewe aitwae Annie.
Kwa mujibu wa gazeti la The Sun la nchini England, babu huyo mwenye
umri wa miaka 65 amelazimika kutengana na mkewe kutokana na maamuzi
yaliyotolewa na mahakama jijini Paris nchini Ufaransa.
Amri ya mahakama imetolewa siku za hivi karibuni na imemtaka Arsene
kuendelea kumuhudumia mwanamama huyo ikiwa ni pamoja na kugawana mali
zisizohamishika na zile zinazohamishika.
Pamoja na yote hayo kutokea wawili hao tayari walikua wameshazaa
mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 18, ambaye atakua na uhuru wa
kuchagua aishi na nani katika kipindi hiki kutokana na umri wake
kumruhusu kufanya lolote.
Balaa lililosababisha ndoa ya Wenger kuvunjika linatajwa kuwa ni
mahusiano ya kimapenzi yaliyokua yakiendelea kati yake na msanii wa
muziki wa kufoka nchini Ufaransa aitwae Sonia mwenye umri wa miaka 39.
Mahusiano hayo yalibainika siku chache kabla ya Arsene Wenger
hajafunga ndoa na Annie mwaka 2010, baada ya kuishi nae kwa muda mrefu
kama rafiki yake ya kike.
Post a Comment