Inawezekana sana kuwa historia kati ya Rihanna na R&B superstaa Chris Brown inawasumbua watu wengi ambao wanania ya kuwa na Rihanna kimapenzi.
Rapper Travis Scott na Rihanna wamekuwa
wakionekana pamoja mara nyingi na sehemu mbalimbali lakini kuna stori
imenifikia inasema kuwa rapper huyo hataki kuhalalisha mahusiano yake na
staa huyo wa muziki mpaka pale atakapo pata baraka kwa aliyekuwa mpenzi
wake wa zamani Chris Brown!
Travis Scott amesema anampenda sana Rihanna na anataka awe na mahusiano ya kudumu kwa muda mrefu na msanii huyo lakini anaogopa kuharibu urafiki wake na Chris Brown
kwasababu ya kitu kimoja tu… anaamini kuwa itakuwa kosa kubwa sana
kutembea na msichana aliewahi kuwa mpenzi wa mshikaji wake wa karibu
sana, hivyo angependa Chris Brown abariki mahusiano hayo.
>>> “namjua
vizuri sana Chris… ni mtu wa hisia na hasira sana, na najua hii ni
historia ya zaidi ya miaka 4 lakini Chris bado anahisia fulani kwa
Rihanna… na nisingependa kuwa na issue zozote na Chris Brown kwasababu
ya ukaribu wangu na Rihanna”. <<< Travis Scott.
Travis amesisitiza kuwa anataka Chris abariki
mahusiano hayo sio kwa kuwa anamuogopa bali ni kwa heshima kati ya
marafiki wawili wenye uhusiano kama mtu na kaka yake… isitoshe Travis na Rihanna wameshaliongelea suala la Chris Brown na Rihanna amemwambia licha ya tofauti zao Chris ni mtu special sana kwenye maisha yake kwahiyo Travis angependa kuwa na amani na Chris wakati yupo na Rihanna kimapenzi.
Post a Comment