Rapa Joh Makini ameeleza sababu zilizomfanya ajiweke kando na kampeni
za siasa kama msanii kwa kufanya shows kwenye mikutano ya kampeni.
Rapa huyo ameeleza kuwa heshima yake kwa mashabiki wa itikadi zote na
dini zote ndio sababu kubwa inayomfanya aache kujiunga na kampeni hizo
ili asiwatenganishe.
“Nina mashabiki kutoka vyama vyote, vile vile nina mashabiki kutoka
dini zote, kwahiyo najaribu pia kuepuka kuwatenganisha,” aliiambia
Clouds FM.
Hata hivyo Joh Makini aliongeza kuwa wasanii walioamua kufanya kampeni hawajakosea kwa kuwa wako kazini na wanafanya biashara.
“Kwa sababu mimi kama msanii ni mfanyabiashara end of the day
ukinilipa hela yangu, nije ni perfome nyumbani kwako sebuleni au kwenye
kampeni yako, mimi nikija pale nitafanya yangu na mwisho wa siku hao
wanaopiga kelele, hawajui kwamba hakuna mtu anaweza kukataa kufanya kazi
yake akilipwa. Mwisho wa siku kama mtu ameenda kufanya show na amelipwa
hela yake hiyo ni haki yake,” Joh alifafanua.
Post a Comment