Kocha wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho ambaye ni mtaalam wa kucheza na saikolojia za makocha na wachezaji wa timu pinzani ili aweze kushinda, kwa sasa yupo katika wakati mgumu na klabu yake ya Chelsea kwani bado haijafanya vizuri katika michezo ya Ligi Kuu.

Licha ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Uingereza msimu uliyopita, klabu ya Chelsea chini ya kocha Jose Mourinho imecheza mechi 5 za Ligi Kuu Uingereza na kushinda moja, sare moja na kupoteza mechi tatu. Hivyo September 15 katika Press Conference na waandishi wa habari, Jose Mourinho ameongea kuhusu hali ilivyo katika vyumba vya kubadilishia nguo.
481302717-467652
” Hili ni swali ambalo limeendelea kuulizwa mara kwa mara lakini jibu ambalo utataraji ni lile lile, hali za wachezaji katika vyumba vya kubadilishia nguo ni kuwa kuna wakati wa kutabasamu na kutaniana nafikiri hilo ni jibu la msingi. Kama watu hawapati mafanikio unatakiwa mpambane ili mfanikiwe nakuahidi tunafanya kazi kwa bidii”>>> Mourinho
“Tatizo pekee tulionalo ni mfululizo wa kutopata matokeo mazuri tunajua na hatufurahishwi na hii hali, ila unaweza kuniuliza kwa nini makocha wengine hawapo katika wakati mgumu licha ya kutofanya vizuri kwa miaka mitano, saba au kumi? lakini mimi bado ni bingwa wa Ligi Kuu Uingereza kwa nni nipate wakati mgumu”>>> Mourinho
MADRID, SPAIN - APRIL 30:  Jose Mourinho, coach of Real Madrid looks on during the La Liga match between Real Madrid and Real Zaragoza at Estadio Santiago Bernabeu on April 30, 2011 in Madrid, Spain.  (Photo by Julian Finney/Getty Images)
Hayo ni baadhi ya majibu ya kocha wa Chelsea Jose Mourinho ambaye amejibu kuhusu yeye kuwa na wakati mgumu kwa sasa, hizo ni kauli zilizotoka wakiwa wanaelekea kucheza mechi yao ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Maccabi Tel Aviv September 16.

Post a Comment