Msanii wa bongo fleva, Nay wa Mitego amemvaa mjumbe wa kamati ya Kampeni ya CCM,January Makamba na kudai yeye ni mnunuaji mkuu wa tafiti na wasanii kwa lengo la kukisaidia chama chake.
Nay
alimjibu January Makamba aliyepost ujumbe ukionyesha kushangaa
tuhuma dhidi ya CCM kuwa imekuwa ikinunua wanasiasa,tafiti
pamoja na wasanii kwa lengo la kuulaghai umma.
"Zitto kanunuliwa. Slaa kanunuliwa. Lipumba kanunuliwa. Twaweza
imenunuliwa. Synovate imenunuliwa. Wasanii wamenunuliwa. Tuwe creative
kidogo" Aliandika January Makamba.
"Ni kabisaa kwani uongo? We ndo mnunuzi mkuu. Bro kama ubunifu ni hela basi we Master wa Ubunifu... @JMakamba Ongeza ubunifu bro" Alijibu Nay wa Mitego
Mpekuzi blog
Post a Comment