Timbulo ni moja kati ya wasanii walioonesha milengo yao kisiasa
mwaka huu, Hit maker huyu wa ‘Domo langu’ ameonekana kwenye ‘stage’ za
UKAWA mara kadhaa.
Akizungumza kupitia kipindi cha The jump off cha Times FM, timbulo
ameelezea mtazamo wake kuhusiana na kitendo cha wasanii wa filamu Aunt
Ezekiel na Vicent ‘Ray’ Kigosi kuhama UKAWA walikokuwa wakishabikia
mwanzoni kwenda Chama cha mapinduzi CCM.
Mkali huyo amesema haikumshitua sana, kwa kuwa matukio kama haya yamekuwa yakijitokeza mara kadhaa.
“kila mtu ana maamuzi yake, wao wamefanya wanachoona kina manufaa
kwao, ila wananchi wanataka mabadiliko, amesaliti Slaa, Lipumba sembuse
wao? haijaniumiza hata kidogo, aliyeniumiza ni Slaa niliyepoteza kura
yangu 2010 kwa ajili yake” alisema Timbulo.
Post a Comment