Usifanye Haya 5 Kama Unaipenda Ndoa Yako
Wanawake wengi wamejenga mazoea ya kufanya baadhi ya mambo niliyoyaorodhesha katika mada hii, mambo amabayo huwapelekea waonekane kuwa ni wanawake wasiofaa kwa waume zao na matokeo yake huzivunja ndoa zao. Kama wewe ni mwanamke uliye katika mapenzi na marakwamara umekuwa ukipokea lawama zifuatazo kutoka kwa mwenza wako ni muhimu kujipa muda wa kujichunguza na kujiweka sawa hasa kama unapenda maendeleo ya penzi lako.TAMU NYINGINE: Adhabu Kubwa Ya Mpenzi Anayekusaliti
Yafuatayo ni Mambo 5 usiyopaswa kuyafanya mwanamke hasa kama unaipenda ndoa yako
1. Usijizuie kuomba msaada kutoka kwa mpenzi wako
Wanawake wengi hujaribu kufanya mambo mengi wenyewe na kukataa kuomba msaada kutoka kwa waume zao hata kama ni dhahiri wanahitaji msaada. Hii hutokea mara nyingi kwa sababu ya fikra zao, kwani wanawake wengi wanatumaini kuwa waume zao wanapaswa kujua nini wanataka na wakati gani wanataka, lakini mapenzi hayafanyi kazi kwa njia hiyo. Hivyo ni muhimu kujifunza kuomba msaada.2. Kuzisambaza Dosari za mume kwa watu wengine
Takwimu zinaonyesha kuwa wanawake wengi hupendelea kuzisambaza dosari za waumezao kwa matumaini kuwa ndio njia pekee ya kuurekebisha mwenendo mbaya wa mume, jamabo amabalo hupelekea dunia kumuona mume hafai kutokana na picha ya sifa mbaya inayosambazwa na mke. Hivyo dunia inajiaminisha ubaya ama udhaifu wa mumeo kutokana na picha uliyomvika machoni pa watu.TAMU NYINGINE: Adhabu Kubwa Ya Mpenzi Anayekusaliti
3. Kutokuwa muwazi kuhusu ‘hisia’ zako
Kila mke anapaswa kujifunza jinsi ya kuwa mwaminifu kuhusu hisia zake. Kuficha mambo yanayokuumiza ni hatari kwa ndoa yako. Kama unajisikia vibaya juu ya jambo fulani alilokufanyia mumeo ni vyema sana kujifunza kuzungumza naye kwa utulivu badala ya kuliweka moyoni na kujifanya kuwa uko sawa kumbe una dukuduku moyoni. Yawezekana hajatambua kabisa kama amekukosea na kama hautomwambia unatarajia afahamu kwa njia ipi?. Unapaswa kutambua kuwa kama utamwendea mumeo kwa utaratibu na kumweleza jambo linalokukwaza atakuelewa tu, badala ya kulificha na matokeo yake unaanza kumchukia bure mumeo.Usifanye Haya 5 Kama Unaipenda Ndoa Yako
4. Kutojali mahitaji yako
Si vibaya kutoa kipaumbele katika mahitaji mbalimbali kwaajili ya familia na watu wengine. Lakini tabia hii isiwe ya kupita kiasi, hata ikupelekee kukujengea fikra mbaya ya kwamba wengine ni bora zaidi kuliko wewe. Ukweli ni kwamba hata ukijinyima kiasi gani hauwtoweza kukidhi mahitaji ya kila mtu. Kinachotakiwa ni kuwa na kiasi katika maamuzi yako kwani ukiiendekeza tabia hii utaishia kupata magonjwa ya moyo bure.TAMU NYINGINE: Adhabu Kubwa Ya Mpenzi Anayekusaliti
5. Usithubutu kumtamkia mumeo kuwa “HUNA HAJA NAYE”
Bila kujali nini kimetokea ama umekakasirika kiasi gani usithubutu kumtamkia mumeo kuwa huna haja naye. Hakuna mtu anayesema kuwa maisha yako yanategemea uwepo wa mume pekee lakini mume anapenda sikuzote kuwepo kwaajili yako na hivyo anapenda kujisikia kuwa na yeye pia ni mtu muhimu sana kwako. Muonyeshe mpenzi wako kuwa unamuhitaji inatosha sana kumtia moyo hasa katika magumu mbalimbali ya kimaisha.Usifanye Haya 5 Kama Unaipenda Ndoa Yako
Post a Comment