Rapa wa Weusi, Nicki wa Pili amesema kuwa kundi hilo halikuwa na
lengo la kuwaeleza mashabiki wake kuhusu collabo kati ya Joh Makini na
mkali wa ‘Skelewu’, Davido.
Hata hivyo, Davido alikuwa mtu wa kwanza kuweka hadharani collabo
hiyo kupitia akaunti yake ya Twitter, huenda baada ya kuona kazi hiyo ni
moja kati ya kazi kubwa ambazo mashabiki wao inabidi wakae mkao wa kula
kukipokea.
“Unajua Davido aliibreak ile news. Sisi tulitaka iwe kimya kimya,
ilikuwa bado iko undercover. Lakini suddenly Davido alitweet jana na
issue ikaenda viral so tukawa hakuna jinsi, lakini bado sio mbaya,”
alisema Nikki wa Pili.
Alisema kuwa chanzo cha collabo hiyo ni juhudi za Joh Makini mwenyewe
ambaye alikuwa akiifuatilia na kuwasiliana na Davido muda mrefu kuhusu
huo mpango. Aliongeza kuwa bado mambo mengi makubwa yanakuja kutoka
kwenye kundi hilo. Bila shaka ana maanisha collabo nyingi kubwa za
kimataifa.
Weusi wanaendelea kuvuka mipaka na kufanya collabo na wasanii
wakubwa, hivi karibuni Joh Makini alifanya collabo na rapa mkubwa wa
Afrika Kusini, AKA.
Post a Comment