Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Brazil, Carlos Dunga ametaja kikosi
kitakachoanza kampeni ya kusaka nafasi ya kucheza fainali za kombe la
dunia za mwaka 2018 dhidi ya Chile pamoja na Venezuela mapema mwezi
ujao.
Dunga ametaja kikosi chake kwa kumuengua nahodha na mshambuliaji wa
mabingwa hao wa kihistoria duniani, Neymar da Silva Santos Júnior
kufuatia adhabu ya kufungiwa michezo minne iliyotolewa shirikisho la
soka la Amerika ya kusini CAMNEBOL wakati wa fainali za mataifa ya
ukanda huo zilizochezwa miezi mitau iliyopita.
Kikosi kamili kilichotajwa na Carlos Dunga tayari kwa mpambano ya
kuelekea nchini Urusi kusaka ubingwa wa dunia mwaka 2018, upande wa
makipa ni Jefferson (Botafogo), Marcelo Grohe (Grêmio) na Alisson
(Internacional)
Mabeki ni Rafinha (Bayern Munich), Marcelo (Real Madrid), Filipe Luis
(Atlético de Madrid), Fabinho (Monaco), David Luiz (PSG), Miranda
(Inter de Milão), Marquinhos (PSG), Gil (Corinthians)
Viungo: Luiz Gustavo (Wolfsburg), Fernandinho (Manchester City),
Elias (Corinthians), Renato Augusto (Corinthians), Lucas Lima (Santos),
Lucas Moura (PSG), Willian (Chelsea)
Washambuliaji: Douglas Costa (Bayern), Philippe Coutinho (Liverpool), Oscar (Chelsea), Roberto Firmino (Liverpool), Hulk (Zenit)
Brazil wataanza kupambana na Chile mjini Santiago kwenye uwanja wa
Nacional Julio Martínez Prádanos, oktoba 8 na kisha watarejea nyumbani
kuchezana Venezuela oktoba 13 kwenye uwanja wa Castelão, uliopo mjini
Fortaleza.
Post a Comment