Chama
cha walimu Tanzania-CWT- kimeipa siku tisa serikali kutekeleza
makubalino ya kutatua kero mbalimbali za walimu ikiwemo kulipa deni la
zaidi ya shilingi bilioni 19 fedha za mishahara na madai mengine kabla
ya kutoa maamuzi kwa wanachama wake.
Akizungumza na waandishi wa habari, rais wa chama cha walimu
Tanzania Bwana Gratian Mukoba ameita kikao dhidi ya serikali
kitakachofanyika Agosti 28 kiwe cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa
madai ya walimu badala ya mapendekezo, mipango na michakato isiyo na
mwisho na kusisitiza CWT hakipendi kuishinikiza serikali kipindi hiki
cha kuelekea uchaguzi bali itambue inawajibu wa kutekeleza makubalino
yalifikiwa na CWT.
Aidha amesema chama cha CWT kilitegemea serikali kulipa posho ya
madaraka kwa walimu wakuu wa shule na wakuu wa vyuo vya ualimu mpaka
sasa haijatolewa hali inayotengeneza deni la shilingi bilioni 5 kila
mwezi na mwisho wa mwezi huu itaongezeka kufikia bilioni 10, pamoja na
walimu zaidi ya elfu 40 wanaostahili kupandishwa daraja kutopandishwa
katika mwaka huu wa fedha.
Post a Comment