Mgombea  Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk John Magufuli jana alifanya kihoja cha mwaka  jukwaani baada ya kuamua  kupiga ‘push up’ ili  kuthibitisha nguvu na alizonazo kuwatumikia Watanzania akichaguliwa.

Akihutubia wafoasi wa CCM wilayani Karagwe, Magufuli alisema wapo watu wanaosema ‘people’s power (nguvu ya umma) na kutaka hiyo nguvu apewe kwa kuwa anayo nguvu ya kutosha kuwatumikia Watanzania.
“Nina power ya kufanya kazi, Au nipige push up,” alisema Pombe.

 

Hatua ya mgombea huyo kufanya mazoezi ya viungo jukwaani, imevuta hisia za wengi na kuzua mijadala kwenye mitandao ya kijamii.

Post a Comment