Najua nina watu wangu wanataka kufahamu ni nchi ipi inayoongoza kwa Uchumi barani Afrika, sasa basi leo nimekusogezea nchi 5 zinazoongoza kwa Uchumi barani Afrika;
Nafasi ya tano (5) imetajwa ni Morocco
Wanasema Uchumi wa Morocco unategemea zaidi Utalii, sekta ya Mawasiliano, viwanda vya nguo,Kilimo pamoja na miji ya marrakech na Rabat ni moja ya miji inayopokea idadi kubwa ya watalii duniani.
Nafasi ya nne (4) imetajwa ni Algeria
Algeria imeshika nafasi ya nne katika nchi ambazo zinaoongoza kwa kuwa na uchumi mkubwa wa Afrika taifa la kaskazini mwa Afrika imeingia katika orodha hiyo.Na moja kati ya sekta inayoiletea uchumi ni usafirishaji wa Mafuta.
Nafasi ya tatu (3) imetajwa ni Nigeria
Wataalamu wa mambo wanasema Mwaka jana
Nigeria ilishika nafasi ya kwanza lakini uchumi wake umeshuka kwa
kipindi hicho ambapo utawala wa rais wa zamani Goodluck Jonathan
ulikuwa ukimaliza muda wake.Nigeria inategemea sana Mafuta ambayo
yanapatikana kwenye taifa hilo, ukiondoka mafuta pia Nigeria katika
sekta ya Mawasiliano na teknolojia , Burudani hasa muziki na Filamu
zimekuwa na mchango mkubwa sana katika taifa hilo.
Nafasi ya pili (2) imetajwa ni Misri
Misri imetajwa kushika nafasi ya pili
kati ya mataifa matano yenye uchumi mkubwa Afrika na kama isingekuwa
matatizo ya siasa ambayo yametetemesha hali ya amani kwenye taifa hilo
basi huenda ingekuwa ya kwanza.Misri ni moja kati ya mataifa ya kwanza
katika ulimwengu huu na kubuni teknolojia kadhaa ikiwemo, Kilimo,
Hesabu, na Ujenzi.
Nafasi ya kwanza(1) imetajwa ni South Africa
Nigeria ndio ilikuwa imeshika nafasi ya
kwanza katika nchi zinazoongoza kwa uchumi barani Afrika lakini kwa
sasa ni Afrika Kusini chanzo kikubwa cha ubora wake kwenye uchumi ni
biashara ya madini na Utalii.
Post a Comment