Kocha wa klabu ya Chelsea ambaye amekuwa akiingia katika headlines mara kadhaa kutokana na tabia yake ya kupenda kulumbana na kuwatoa mchezoni wapinzani wake kwa maneno yake ya kejeli. September 25 Mourinho amenukuliwa na vyombo vya habari akitoa kauli bila kutaja jina lakini waandishi wanajua alimlenga kocha wa Arsenal Arsene Wenger.

Kauli ya Mourinho inakuja ikiwa ni siku kadhaa zimepita toka klabu ya Chelsea iifunge klabu ya Arsenal kwa goli 2-0  Mourinho bado anaendeleza kauli zake ambazo ni kama ishara ya kumkejeli Wenger licha ya kuwa hakumtaja moja kwa moja ila kauli hii inatafsiriwa kumlenga Wenger.
2C80C82400000578-3249035-image-a-25_1443187316818
“Kila kocha wa Ligi Kuu Uingereza ana presha na Ligi, Steve McClaren, Pellegrini na  Brendan Rodgers wote wana presha na mechi za Ligi na tunalazimika kuyafikia malengo, kiukweli nawaonea huruma kwa sababu ni kazi ngumu. lakini kuna mmoja ambaye hayupo katika hiyo list lakini yeye anajisikia vizuri na wala hana presha”>>> Mourinho
2C9BC47000000578-0-image-a-21_1443186640591
Hii ni picha ya tukio la mechi ya weekend iliyopita Gabriel na Diego Costa waligombana
Kauli ya Mourinho inatafsiriwa imemlenga kocha wa Arsenal Arsene Wenger moja kwa moja kwani ndio kocha ambaye kikosi chake hakifanyi vizuri kwa miaka ya hivi karibuni, hivyo Mourinho anamkejeli Wenger kwa kumtaja kuwa anaweza akafungwa, akalia lakini akaendelea na kazi yake kama kawaida tofauti na makocha wengine ambao kama watafanya vibaya wanaweza fukuzwa kazi.

Post a Comment