Shetta amekanusha tuhuma za kujihusisha na dawa za kulevya maarufu kama ‘Unga’ zilizoelekezwa kwake na watu mbalimbali na kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.


Tuhuma hizo zinachangiwa na jinsi ambavyo mwanamuziki huyo wa Bongo Flava anavyofanya safari za kwenda Afrika Kusini mara kwa mara na kampani ya rafiki zake anaokuwa nao huko.
Shet
“Mimi nafanya muziki wangu na muziki unanifanya nifanye biashara nyingine kwa sababu South Africa inasemekena wasanii wengi wanauza madawa ya kulevya kwahiyo nisiende South Africa,” Shetta ameiambia Clouds Fm.
“Hicho sio kitu cha ukweli, wanasema nakuwa pamoja na watu wanaouza madawa ya kulevya, mimi hawajahi kuniambia wanafanya hiyo biashara na sijui kwanini niingiliwe uhuru wa kuwa na marafiki? Labda ningekuwa nawajua ningewapisha ili wasinichafulie jina,” alitiririka.

Post a Comment