Utafiti
uliofanywa na taasisi inayojisughulisha na masuala ya kitafiti ya
Twaweza umebainisha kuwa chama cha mapinduzi CCM ndio chama
kinachaopendwa zaidi na wananchi kwa asilimia 62.
Akiwasilisha matokeo ya utafiti huo mkurugenzi wa Twaweza Bw Aidan
Eyakuze amesema chama cha demokrasia na maendeleo Chadema ndio chama
kinachoshika namba ya pili kwa kupendwa na watu ingawa utafiti pia
umeonyesha kuwa idadi ya watu wanaosema kwamba watawachagua wagombea wa
Chadema katika ngazi ya urais, ubunge na udiwani imepungua kidogo.
Aliyewahi kuwa mjumbe wa bunge maalum la katiba Bi Maria Sarungi
akitoa maoani yake kuhusu utafiti huo amesema hayo ni matokeo tuu na
wala siyo lazima siku ya mwisho ya kupiga kura hali ibaki kuwa vilevile
bali jambo la msingi ni vyama vya upinzani kuongeza nguvu katika
kujitambulisha kwa umma.
Naye mwenyekiti wa kigoda cha Mwalimu Nyerere Prof Penina Mlama
amesema utafiti huo ni mapema sana kwa sasa kukubali ama kuukataa kwani
kuna vitu vingi vya kuangalia kama vilizingatiwa katika utafiti huo
ambapo Bw Stepheni Robert mwanafunzi wa mwaka wa tatu chuo kikuu cha Dar
es Salaam anayechukua masula ya sheria amesema utafiti huo unamapungufu
chungu mzima ikiwemo kitendo cha kuwapa simu wale wanaohojiwa alafu
utegemee majibu tofauti.
Post a Comment